Ni wakati wa CCM kusikiliza kero na sio kutoa hotuba - Makonda
Eric Buyanza
February 8, 2024
Share :
Katibu wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi Taifa, Itikadi,Uenezi na Mafunzo,Paul Makonda amesema kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM)ni chama ambacho kinataka kihangaike na kero za wananchi na sio kutoa hotuba ni wakati wa kushughulikia maisha ya wananchi ambao wanachangamoto mbalimbali zinazowakabili.
Makonda amesema hayo wakati akizungumza kwenye Mkutano wa hadhara na Wananchi katika viwanja vya Ruanda Nzovwe mkoani hapa ikiwa ni mwendelezo wa ziara zake za mikoa 20 katika kusikiliza kero za wananchi.
“Uwe wakati wa chama kiwe na faraja kwa wananchi na matumaini ya kuishi na chama hiki kimeshashinda dora hivyo hakuna sababu ya kusubiri uchaguzi kwasababu kina wajibu wa kuhakikisha kuwa kila mwananchi anapata haki yake” amesema Makonda.