pmbet

Nick Cannon azikatia Bima Korodani zake kwa shilingi Bilioni 26

Eric Buyanza

June 8, 2024
Share :

Muigizaji na mtangazaji wa TV maarufu nchini Marekani, Nick Cannon, ameweka bima ya korodani zake kwa $10m (sawa na shilingi Bilioni 26 za kitanzania).

Cannon ameamua kufanya hivyo baada ya kutimiza idadi ya watoto 12 aliozaa na wanawake sita tofauti.

Gazeti la Daily Mail limeripoti kwamba muigizaji huyo aliishirikisha kampuni ya uuzaji wa bidhaa za kiume (Dr. Squatch), ambayo ilizifanyia tathmini korodani hizo kabla ya kuzikatia Bima.

Kwenye taarifa yake, Nick alisema: "Wanaochukia wanasema ni wakati wa mimi kuacha kuendelea kuzaa, lakini nimeamua kuongeza maradufu thamani ya korodani zangu na watoto wangu wa baadae.

“Pongezi kwa Dk. Squatch kwa kuzipa korodani zangu sifa inayostahili na kuniunganisha na ulinzi ninaohitaji ili kuendeleza mti wa familia” 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet