Nick Minaj aandaa bonge moja la Tour
Eric Buyanza
December 15, 2023
Share :
Baada ya kuachia album yake ya ‘Pink Friday 2’ na kufanya vizuri wiki iliyopita, rapa wa kimarekani Nick Minaj ameachia rasmi orodha ya sehemu atakazozunguka na kufanya ziara maalum ya Album hiyo ifikapo mwaka 2024.
Ziara hiyo ambayo imepewa jina la ‘Nicki Minaj Pink Friday 2 Tour’ inatarajiwa kuanza Machi mosi mwaka 2024 katika mji wa Oakland, Calirfonia na kutamatika Juni 7, Berlin.