Nicki Minaj awa Rapa wa kwanza wa kike kufikisha 'streams' Bilioni 1
Eric Buyanza
March 1, 2024
Share :
Malkia wa Rap Nicki Minaj kutoka nchini Marekani amejiweka kwenye historia ya muziki itakayoendelea kusomwa baada ya kufanikiwa kuwa Rapa wa kwanza wa kike kufikisha 'streams' bilioni moja kwenye mtandao wa Spotify mwaka huu 2024.
Nyingi ya 'streams' hizo zimetoka kwenye albam yake 'Pink Friday 2' aliyoiachia mwishoni mwa mwaka jana huku zingine zikitoka kwenye single mpya 'Big Foot' iliyotoka mwanzoni mwa mwaka huu.
Nicki ambaye jina lake halisi ni Onika Tanya Maraj, baadaye mwaka huu anatarajiwa kuanza ziara (tour) kwa ajili kupromote albam yake ya ‘Pink Friday 2’