Nicki Minaj aweka historia ya kuwa Rapa wa kike aliyefanikiwa zaidi kwenye ziara
Eric Buyanza
April 9, 2024
Share :
Malkia wa Rap, Nicki Minaj amevunja rekodi ya ziara iliyoingiza pesa nyingi zaidi kwa rapa wa kike katika historia.
Kulingana na kampuni ya takwimu ya Marekani, Touring Data, nyota huyo wa muziki wa hip-hop mwenye makazi yake nchini Marekani, ameweka rekodi ya kuwa rapa wa kike katika historia aliyefanya tamasha lililoingiza mkwanja mrefu zaidi, dola milioni 2.858 kwenye kwenye ukumbi Madison Square Garden huko New York Machi 30, 2024.
Ziara yake ya ‘Pink Friday 2’ imekuwa ziara iliyofanikiwa zaidi kwa rapa wa kike, ikiingiza dola milioni 34.9 kutokana na tiketi 220,000 zilizouzwa katika show zake 17 za kwanza.
"Pink Friday 2" ya @NICKIMINAJ inakuwa rasmi ziara yenye mafanikio zaidi ya rapa wa kike katika historia, ikiwa na $34.9 milioni kutoka kwenye tiketi 220,000 zilizouzwa katika maonyesho yake 17 ya kwanza," Touring Data iliandika kwenye ukurasa wake wa X (zamani Twitter).
Alipata $34.9 milioni kutokana na asilimia 30 tu ya ziara hiyo. Anatarajiwa kuingiza dola milioni 100 mwishoni mwa ziara hiyo baadaye mwaka huu.