Nicki Minaj kuutosa muziki wa Hip-hop?
Eric Buyanza
July 9, 2024
Share :
Unaweza usiamini lakini Rapa mwanadada Nicki Minaj baada ya kunogewa na shangwe alilopata huko nchini Austria ametamani kuuweka pembeni muziki Hiphop ili afanye zaidi muziki wa mahadhi ya Pop.
Minaj alidokeza hilo hivi karibuni alipokuwa kwenye tamasha lake huko jijini Vienna nchini Austria, baada ya kuona jinsi mashabiki wa nchi hiyo walivyoupokea kwa shangwe la kibabe wimbo wake wa mahadhi ya Pop uitwao ‘Starships.
Wimbo 'Starships' una takriban miaka 12 tangu utoke.
Nick Minaj anachukuliwa kuwa mwana hip-hop bora zaidi wa kike wa muda wote.