Nico Williams kuungana na Lamine Yamal Barcelona
Sisti Herman
July 4, 2024
Share :
Winga hatari wa klabu ya Athlethic Bilbao Nico Williams ameonyesha nia kubwa ya kujiunga na klabu ya Barcelona kwaajili ya kuichezea kuanzia msimu ujao.
Akiwa na Bilbao msimu ulioisha majuzi, Nico amecheza mechi 31 amefunga goli 5 na asisti 11 huku akiingia kwenye timu bora ya wiki mara 5 tofauti kwa muibu wa Sofascore.
Kama endapo Nico atajiunga na Barcelona ataungana na rafiki zake wa timu ya Taifa kama Lamine Yamal na Pedri.