Nico Williams na Pino huenda wakakosa mechi zilizosalia
Eric Buyanza
June 27, 2026
Share :
Winga wa timu ya taifa ya Uhispania na klabu ya Crystal Palace, Yeremy Pino, yuko hatarini kukosa mechi zote zilizobaki za Kombe la Dunia.
Pino amepata jeraha la kuvunjika kwa mfupa wa 'collarbone' uliopo begani. Jeraha hili lilitokea baada ya kuanguka vibaya akicheza dhidi ya Uruguay.
Kocha mkuu wa Uhispania, Luis de la Fuente, amethibitisha kuwa kuna uwezekano mkubwa sana akalazimika kukosa mashindano yote yaliyosalia kutokana na ukubwa wa maumivu na jeraha lenyewe.

Kwa upande wa Nico Williams, yeye pia anaweza asicheze tena kwa muda uliobakia wa mashindano hayo kwa kuwa hali yake inatia mashaka kufuatia kupata jeraha kwenye msuli wa paja kwenye mchezo huohuo dhidi ya Uruguay.
Williams aliingia kipindi cha pili lakini alimaliza mechi hiyo akiwa anachechemea vibaya na kuonyesha dhahiri kuwa ana maumivu makali.





