pmbet

Nigeria hawaamini macho yao, wakati Tyla akiibeba Afrika

Eric Buyanza

February 5, 2024
Share :

Ulikuwa ni usiku ambao hautasahaulika kwa wanigeria wengi na haswa wasanii waliokuwa kwenye kinyang'anyiro cha kuwania tuzo za Grammy kwa mwaka 2024 baada ya kuambulia patupu.
 

Ni mwaka ambao Wanigeria walijiamini kuwa lazima wangeambulia kitu kwnye tuzo hizo za 66 za Grammy 2024 zilizofanyika usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa Crypto.com Arena Jijini Los Angeles nchini Marekani.
 

Burna Boy, mshindi wa Grammy 2021 ndiye msanii wa Nigeria na Afrika aliyechaguliwa kuwania vipengele vinne, Davido vitatu, huku Asake na Ayra Starr wakipata kimoja kimoja.
 

Mkali wa ngoma 'Last Last' Burna Boy alitajwa vipengele vya Best Global Music Album (I Told Them), Best African Music Performance (City Boys), Best Global Music Performance (Alone) na Best Melodic Rap Performance (Sittin' on Top of the World).
 

Naye Davido ambaye ni mara yake ya kwanza kuwania Grammy alitajwa vipengele vya Best Global Music Album (Timeless), Best Global Music Performance (Feel, Unavailable) na Best African Music Performance.
 

Hata hivyo, Burna Boy, Davido na wenzao wameambulia patupu katika vipengele vyote na sasa watarejea nyumbani kwao bila kitu chochote ambacho hata mashabiki na wadau wao hawakukitarajia hapo awali.
 

Staa wa Amapiano kutokea Afrika Kusini, Tyla, wa ndiye msanii pekee wa Afrika aliyeibuka mshindi wa Grammy 2024, ambapo ameshinda kwenye kipengele cha 'Best African Music Performance' baada ya kuwabwaga Asake, Burna Boy, Davido na Ayra Starr.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet