pmbet

Nigeria yatinga Ikulu kumuomba radhi Ibrahim Traoré

Eric Buyanza

December 18, 2025
Share :

Nigeria imeiomba radhi Burkina Faso kufuatia ndege yao kuruka kwenye anga la nchi hiyo bila idhini wiki iliyopita. 

Waziri wa Mambo ya Nje wa Nigeria, Yusuf Maitama Tuggara jana Desemba 17 alikuwa mjini Ouagadougou na alipokelewa Ikulu na kiongozi wa nchi hiyo Kapteni Ibrahim Traoré. 

Yusuf alisema alikuwa amebeba ujumbe wa "mshikamano na udugu" kutoka kwa Rais Ahmed Bola Tinubu wa Nigeria kwa mwenzake wa Burkina Faso, aliomba radhi kwa niaba ya nchi yake akisema: 

"Inasikitisha kuona kulikuwa na ukiukwaji wa sheria. Hii ni bahati mbaya, na tunaomba radhi kwa tukio hili baya."

Wiki iliyopita, ndege ya kijeshi ya C-130 ya Nigeria ililazimika kutua kwa dharura huko Bobo-Dioulasso, Burkina Faso, ingawa haikuwa na idhini ya kuruka juu ya anga ya Burkina Faso.

Wafanyakazi 11 walikamatwa. Kulingana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Nigeria, bado wako Burkina Faso na wanahudumiwa vizuri.

Hata hivyo, waziri hakutoa maelezo yoyote kuhusu uwezekano wa kuachiliwa kwao au kurejeshwa kwa ndege hiyo.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet