"Niko hai na ni mzima", Ngozi Ezeonu akanusha uvumi wa kifo
Eric Buyanza
January 11, 2024
Share :
Muigizaji mkongwe wa Nollywood, Ngozi Ezeonu amekanusha taarifa kuwa amefariki.
Kupitia video aliyoitupia kwenye mtandao wake wa kijamii muigizaji huyo alisema "Yuko hai na mwenye Afya".
Alikuwa akijibu tetesi zilizoenea kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuwa amefariki.
“Katika uandishi wa habari, unachofanya ukiwa na mashaka na habari fulani ni kuachana nayo ikiwa huwezi kumfikia muhusika angalau kuthibitisha habari hiyo."
“Huu ni mwaka mpya, kwa nini mtu atake kuumiza mwenzake kwa sababu tu ya kutaka followers?”aliuliza mwanamama huyo anayekubalika sana kwenye soko la Tanzania.