'Niko katika hali nzuri', Biden atetea afya yake, asema msiwe na hofu
Eric Buyanza
July 13, 2024
Share :
Rais wa Marekani Joe Biden alirejea kwenye kampeni siku ya Ijumaa akiendelea kuwahakikishia wapiga kura na wanachama wa chama chake cha Democrat kuwa anastahili kuendelea kuwa madarakani pamoja na kelele nyingi zinazomtaka ajiondoe kwenye kinyang'anyiro cha kugombea Urais kwa mara nyingine.
DW inaripoti kuwa akiwa mjini Northvillle katika jimbo la Michigan, Biden amewahakikishia wafuasi wake kwamba yuko vizuri na kwamba ni lazima amshinde mpinzani wake Donald Trump katika uchaguzi wa nchi hiyo utakaofanyika Novemba 5 mwaka huu.
Hata hivyo kelele za wanachama wa Democrat zinazomtaka ajiondoe zinazidi kuongezaka, huku wabunge 19 wa chama chake wakimtaka waziwazi asigombee tena uchaguzi kufuatia kushindwa kwake vibaya katika mdahalo dhidi ya Trump Juni 27.
Akiwa kwenye mkutano wa jumuiya ya kujihami NATO uliofanyika wiki hii, Biden alikosea na kumuita makamu wake Kamala Harris, kwa jina la 'Trump' na baadaye pia akamuita rais wa Ukraine Volodymir Zelensky kwa jina la 'Putin.
Mfululizo wa matukio hayo unaongeza shinikizo juu ya uwezo wake wa kiakili ingawa yeye anasisitiza kuwa yuko sawa.