pmbet

NIKO KWENYE ORODHA YA KIFO YA URUSI: Bosi wa kampuni ya Droni alalama

Eric Buyanza

September 18, 2026
Share :

Stefan Thumann, mkuu wa kampuni ya Ujerumani inayoiuzia Ukraine droni za mashambulizi, amesema anaishi mafichoni baada ya mamlaka kumwonya kuhusu njama inayodaiwa kutoka Urusi ya kutaka kumuua.

 

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya teknolojia ya ulinzi ya Donaustahl, Stefan Thumann, amesema amelazimika kuishi mafichoni kutokana na kile kinachodaiwa kuwa mpango wa Urusi wa kumuua.

 

Thumann, mwenye umri wa miaka 39, amesema hubadilisha makazi kila baada ya majuma kadhaa na huandamana wakati wote na walinzi binafsi. Alizungumza na Shirika la Habari la Ufaransa, AFP, kutoka eneo ambalo halikufichuliwa.

 

Kwa mujibu wake, mamlaka zilimwonya mwezi Desemba mwaka jana kuwa maisha yake yako hatarini. Baadaye alielezwa kuwa kitisho hicho kinadaiwa kutoka Urusi na kwamba kulikuwa na mpango wa kujaribu kumuua.

 

Thumann ni mfuasi wa wazi wa Ukraine katika vita vyake dhidi ya Urusi.Kampuni yake yenye makao yake katika jimbo la Bavaria hutengeneza na kuuza droni za mashambulizi kwa Kyiv.

 

Amesema kuishi mafichoni kumebadilisha maisha yake kabisa. Bado anasimamia shughuli za Donaustahl, lakini mawasiliano yake na familia ni machache na hufanyika kwa njia za kidijitali pekee.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet