pmbet

Niko tayari kumkabili mdosi – Kiduku

Eric Buyanza

April 4, 2024
Share :

Bondia wa ngumi za kulipwa kutoka Mkoani Morogoro, Twaha Kiduku, amesema ameshakamilisha maandalizi yake kwa kiwango kikubwa na yupo tayari kwa pambano dhidi ya bondia Hapreet Sigh kutoka nchini India.

Pambano hilo la kimataifa lisilokuwa la ubingwa lililopewa jina la ‘Hatukimbii Hatuogopi’ linatarajia kupigwa tarehe 11/04/2024 kwenye ukumbi wa Tanzanite, mkoani Morogoro.

“Mimi pamoja na timu yangu tuko vizuri kiafya na kila kitu, naamini siwezi kuwaangusha Watanzania. Hakuna ugomvi rahisi, siku zote ugomvi ni ugomvi kikubwa ni kujiandaa na kumheshimu mpinzani,” amesema Kiduku.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet