pmbet

Niko tayari kuolewa mke wa pili - Tiwa Savage

Eric Buyanza

October 20, 2025
Share :

Mwanamuziki wa Nigeria, Tiwa Savage amefunguka kuhusu hali anayopitia kimahusiano huku akisema wanaume wengi ambao anawaelewa wako kwenye umri wa miaka 50 au wameoa tayari.

Tiwa aliyasema hayo hivi karibuni alipokuwa akiongea kwenye 'podcast' ya Air Service ya nchini Marekani;

"Kila ninayekutana nae ambaye angeweza kunioa, utakuta yupo kwenye umri wa miaka 50 au tayari ameshaoa. Kwa hivyo, sijui! Labda naweza kuwa mke wa pili. Nafikiri hivyo. Ninaweza kuwa mke wa pili," alisisitiza.

"Nadhani naweza kwenda sambamba na mke wa kwanza na akanipenda kwa sababu sitakuwa msumbufu. Nitakuwa nikienda kwenye ziara zangu, sitamsumbua kabisa. Nina heshima sana, najua kuwa wewe ni mke wa kwanza na nitakupa heshima hiyo" alimalizia msanii huyo.

Mwaka 2013 Tiwa Savage alifunga ndoa na Tunji Balogun almaarufu Tbillz, ambapo ndoa hiyo ilivunjika mwaka 2018 baada ya kila moja kumshutumu mwenzake kwa usaliti.

Wawili hao wana mtoto mmoja wa kiume.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet