pmbet

Nilianza maisha yangu ya soka kama golikipa - Benjamin Sesko

Eric Buyanza

February 14, 2026
Share :

Benjamin Sesko amefunguka namna alivyofikia kuwa mshambuliaji mahiri, akisema kwamba alianza maisha yake ya soka kama golikipa.

 

Akizungumza kwenye podcast ya Inside Carrington Sesko alisema:
 

"Nilianza kama kipa nikiwa na umri mdogo sana. Lakini nakumbuka siku moja katikati ya mchezo nilimtazama baba yangu nikasema “Baba ninaboreka sana...sina chochote cha kufanya nikiwa golini."

"Ilikuwa vigumu kwangu kuangalia wachezaji wenzangu wakicheza na wakashindwa kufunga... kuna wakati nikiwa golikipa nilikuwa nachukua mpira napita nao uwanja mzima kisha nafunga.”

"Kwa hakika ilikuwa safari nzuri.....nilianza kama beki wa kati na kisha nikapanda na kuwa mshambuliaji" anasema mchezaji huyo raia wa Slovenia.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet