Nilifanya uamuzi sahihi kuondoka Barcelona kwenda PSG - Dembele
Eric Buyanza
June 13, 2026
Share :
Fowadi wa Ufaransa, Ousmane Dembele, amesisitiza kwamba alifanya uamuzi sahihi kuondoka Barcelona na kwenda Paris Saint-Germain miaka michache iliyopita.
Dembele alijiunga na Barcelona mwaka 2017 na kukaa miaka sita na mabingwa hao wa LaLiga.
Alipoulizwa kama uamuzi wake wa kuondoka katika klabu hiyo ya Catalan kwenda PSG ulikuwa ni uamuzi bora kwenye maisha yake ya soka, Dembele aliliambia gazeti la Marca: "Ndiyo, nadhani hivyo...kwa upande wangu, nadhani ulikuwa ni wakati mwafaka wa kuondoka klabuni hapo. Ingawa nilikuwa nikiipenda sana Barca, ambayo nimekuwa nikiiunga mkono tangu nikiwa mdogo."






