pmbet

Niliingia kwenye muziki kwasababu ya mwanaume

Eric Buyanza

April 17, 2024
Share :

Mwanamuziki wa Kinigeria mwanadada Tiwa Savage amesema alilazimika kuingia kwenye muziki kwasababu ya mwanaume aliyekuwa akimpenda...lakini moyoni mwake alichokuwa akikipenda zaidi ilikua ni uigizaji.

"Siku zote nilitaka kuwa muigizaji, uigizaji ulikuwa mojawapo ya ndoto zangu za kwanza kabla ya muziki” anasema Tiwa.

“Niliingia kwenye muziki kwa sababu nilikuwa na mapenzi na jamaa fulani ambaye alikuwa karibu sana na mwanamuziki....nikaona niachane kuigiza niingie tu kwenye muziki”

Tiwa alifichua siri hiyo wakati akizungumzia ujio wa filamu yake mpya "Water and Garri" inayotazamiwa kutikisa soko la filamu la Nollywood.

Filamu hiyo ya kwanza kwa msanii huyu imetayarishwa na kampuni ya mwanadada huyo iitwayo 'Everything Savage' akishirikiana na Unbound Studios.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet