"Nilikuja Uturuki kujenga historia mpya" – Mo Salah
Eric Buyanza
November 10, 2026
Share :

Mshambuliaji wa kimataifa wa Misri na klabu ya Trabzonspor, Mohamed Salah, amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu sababu zilizomfanya kuchagua kujiunga na Ligi Kuu ya Uturuki (Süper Lig), huku akizikataa ofa nono kutoka Saudi Pro League pamoja na klabu kubwa barani Ulaya.
Salah, ambaye alijiunga na Trabzonspor msimu huu akitokea Liverpool, amesema uamuzi wake uliongozwa na hamu ya kupata changamoto mpya na ya kipekee, badala ya kwenda kwenye timu zilizosheheni mastaa tayari.
Katika mahojiano yake hivi karibuni, "Mfalme huyo wa Misri" alisema;
“Najua kulikuwa na watu walionitegemea kuniona katika ligi ya Saudi Arabia au kwenye moja ya klabu kubwa Ulaya, lakini mimi niliona kitu cha tofauti kabisa ndani ya Trabzonspor. Nilitaka changamoto mpya, lakini si mahali ambapo mastaa tayari wamejazana, kwa sababu kuna kitu nataka kukijenga hapa.”





