Nilikunywa juice mara ya mwisho mwaka 2,000
Eric Buyanza
February 22, 2024
Share :
Akiongea akiwa jijini Mwanza, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Profesa Mohamed Janabi amesema anaigopa sana juice kwa sababu ya sukari.
“Ukinywa glass moja asubuhi machungwa matano, mchana matano na jioni matano maana yake kwa mwezi ni machungwa 450, unaharibu afya yako, ogopa zaidi vitu vitamu tamu, unavyozungumzia sukari sio sukari tu bali ni vitu vitamutamu. Pale Muhimbili tunao watoto wa miaka tisa wana kisukari, mimi naogopa sana juice nafikiri mara ya mwisho nimekunywa mwaka 2000” amesema Profesa Janabi