"Nilikuwa mzinzi lakini nimemrudia mungu wangu" - Cassper Nyovest
Eric Buyanza
February 12, 2024
Share :
Rapper wa Afrika Kusini, Cassper Nyovest amefichua kuwa upendaji wa ngono uliopita kiasi ndio chanzo cha kuachana na mama watoto wake, Thobeka Majozi.
Ikumbukwe kuwa wawili hao wana mtoto wa kiume waliyempata Septemba 2020.
Akiongea kwenye mahojiano aliyoyafanya hivi karibuni kwenye Podcast ya Mpoomy Ledwaba, Cassper alikiri kuumiza hisia za mama watoto wake huyo walipokuwa kwenye mahusiano.
Hata hivyo, alifichua ya kwamba kwasasa ameokoka na ameamua kumrudia mungu wake.
"Nilimuumiza sana mama mtoto wangu. Tuliachana, na nimekuwa single kwa miaka miwili, Nilikuwa muasherati na mbinafsi mkubwa na nilijiona kuwa bora kuliko wengine" rapper huyo alisema.