pmbet

Nilikuwa na pesa kabla hata sijaingia kwenye muziki

Eric Buyanza

February 16, 2024
Share :

Mwanzilishi wa muziki wa Takeu, Lucas Mkenda maarufu Mr. Nice amesema sanaa ya uchoraji ndiyo iliyoanza kumuingizia fedha nyingi kabla hajaingia kwenye muziki na kuwa maarufu.
 

Mr. Nice amesema mashabiki wake wengi wanadhani alianza kushika fedha nyingi alipokuwa mwanamuziki lakini hawafahamu kama alikuwa na maisha mazuri kabla ya kuingia kwenye muziki.
 

“Watu wengi wanasema nimefulia kwa sababu hawanijui wanasema nimetumia vibaya fedha sasa walitaka nitumiaje? Nilitumia nilichokuwa nikiigiza na pia muziki ilikuwa sehemu nyingine ya mimi kupata fedha lakini kabla ha muziki nilikuwa nachora na kuuza picha kwa wazungu zilikuwa zikinipatia fedha nyingi lakini pia nilikiwa nikiuza duka la mama hivyo nashika fedha nyingi wengi hawajui,” ameeleza Mr Nice.
 

“Nikweli muziki umeniingizia fedha nyingi lakini kabla sijaingia kwenye muziki nilikuwa na kazi nyingine nyingi zilizoniingizia fedha nyingi hivyo kutumia kwa starehe ilikuwa kawaida kwangu kwa kuwa nilikuwa na fedha kabla na nilipoingia katika muziki pia nikawa naingiza fedha nyingi zaidi,” amesema Mr. Nice.
TSN
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet