Nilimuomba Mungu aondoe kila jambo baya kwangu - Wizkid
Eric Buyanza
July 5, 2025
Share :
Mkali wa miondoko ya Afrobeats kutoka Nigeria, namzungumzia Ayodeji Balogun, almaarufu Wizkid, amefunguka akisema alikuwa na mazungumzo ya karibu na Mungu na kuomba kila jambo baya liondolewe katika maisha yake na amekuwa akiona dalili zote kuwa Mungu anajibu maombi yake.
Kutokana na hilo, Wizkid pia amewataka mashabiki zake kumshirikisha Mungu katika mambo yao.