Nilipokutana na mume wangu, alikuwa na wanawake 87
Eric Buyanza
January 20, 2024
Share :
Mwanamke mmoja maarufu nchini Nigeria anayefahamika kwa jina la Adetoun Onajobi, anasema wakati anakutana mume wake kwa mara ya kwanza...alimkuta akiwa na mademu 87.
Mwanamke huyo ambaye pia ni mchambuzi wa mambo ya siasa, anasema kwa kutumia njia anazozijua alifanikiwa kuwakimbiza wanawake hao wote na kuuteka moyo wa mwanaume huyo (kwasasa mumewe).
Wakati wa mahojiano aliyoyafanya hivi karibuni, Adetoun anasema haikuwa vita rahisi kwani ilimpasa kupigana kimwili na kiroho ili kupata ushindi huo.