pmbet

Nilirekodiwa bila kujua, siamini tena wanawake

Sisti Herman

December 27, 2023
Share :

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Gigy Money amefunguka kwa mara ya kwanza kwenye mahojiano maalum na PMTV tangu kutokea kwa sakata lake la mikanda yake ya video za utupu kusambaa mitandao huku akisema kuwa alirekodiwa bila ridhaa yake na video kusambazwa.

 

“Nilirekodiwa bila kujijua, nilifanyiwa unyama, nilidhalilishwa hadharani, kuhisi siwezi tena kumwamini mwanaume, hicho kitu ni kibaya sana na sidhani kama ntakuja kuwa na mwanaume mwaka huu, mwakani au hata milele sawa tu, kwasababu mwanzo hawaji na sura ya kudhamiria kukudhuru, huja na upendo siwezi kusahau” alisema Gigy kwa kusikitika.

 

“Marafiki zangu wengi ni wanaume, ni kama siamini wanawake, niliwahi kuamini mwanamke yakanitokea yaliyotokea lakini wanaume wamenyooka kama ni ukweli wanamwambia mtu ukweli na kama ni uongo unamwambia mtu, sisi wanawake tunazunguka sana halau ukweli ndo wa mwisho, kwahiyo utanikuta na wakaka, dereva wangu, walinzi wangu binafsi” alisisitiza Gigy akipoteza kabisa matumaini na marafiki zake wa kike.

 

Kwa undani zaidi fuatilia mahojiano haya kupitia mtandao wa Youtube wa PMTV

 

 

 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet