Nilisimamisha kazi yangu kwasababu ya penzi - Shakira
Eric Buyanza
March 18, 2024
Share :
Akiongea kwenye mahojiano mwishoni mwa wiki mwanamuziki wa colombia Shakira amedai kuwa kazi yake ya muziki aliipa kipaumbele cha mwisho kwa miaka mingi kwa sababu ya mpenzi wake wa zamani Gerard Piqué (mchezaji wa zamani wa Barcelona).
Shakira ambaye kwasasa ana umri wa miaka 47 anasema...."Kwa muda mrefu nilisimamisha kazi yangu ili kuwa karibu na Gerard, ili aweze kucheza mpira........kulikuwa na kujitolea kwingi kwa ajili ya upendo" aliongeza.
Nyota huyo wa muziki wa Colombia na mchezaji kandanda wa zamani wa Uhispania walikuwa pamoja kwa miaka 11 kabla ya kuachana Juni 2022.
Mastaa hawa wana watoto wawili Milan na Sasha