Nilistahili kuwa mchezaji bora Afrika - Mayele
Eric Buyanza
December 13, 2023
Share :
Mshambuliji wa Pyramids, Fiston Mayele ameandika ujumbe kupitia akaunti yake ya Instagram;
“Hakuna asiyejua kuwa mwaka wa 2023 ni Mayele fulani ambaye anastahili kuwa mchezaji bora anayecheza Afrika, lakini tunaelewa muhtasari licha ya yote niliyozawadiwa na timu yangu kwa zawadi hii yote kwa yote nawashukuru saana mashabiki zangu kwa sapoti na dua zenu nawapenda,” alimalizia.
Tuzo ya mchezaji bora wa mashindano ya klabu ndani ya Afrika iliyotolewa nchini Morocco jana ilichukuliwa na Percy Tau anayekipiga Al Ahly akiwaburuza Mayele na Peter Shalulile.