Nilistahili Tuzo 20 za Grammy - Davido
Eric Buyanza
February 3, 2024
Share :
Msanii Davido kutoka nchini Nigeria amesema mpaka alipofikia alistahili kuwa na Tuzo 20 za Grammy kutokana na ngoma zake kupigwa nchi mbalimbali.
Aliyasema hayo kupitia mahojiano yake na kituo cha runinga cha ‘Farance 24’ baada ya kuulizwa swali kuhusiana na kutajwa kwake kuwania Tuzo za Grammy kuna maana gani?, ndipo akaeleza kuwa alifanya kazi kubwa kwenye albam ya ‘Timeless’, hivyo alistahili kupata Tuzo 20 za Grammy hapo nyuma kama angeitoa mapema.
Ikumbukwe, Davido ametajwa kuwania vipengele vitatu katika Tuzo za Grammy vikiwemo Best Global Music Album (Timeless), Best Global Music Performance (Feel, Unavailable) na Best African Music Performance.
Tuzo hizo zinatarajiwa kutolewa Februari 4, 2024 katika ukumbi wa ‘Crypto.com Arena’ ulioko Los Angeles nchini Marekani.
Hii itakuwa mara ya kwanza kwa Davido kuwania tuzo za Grammy, endapo atashinda atakuwa msanii wa pili kunyakua tuzo hizo. Mpaka sasa Wizkid ndiye msanii pekee wa Afrika aliyewahi kushinda Grammy mwaka 2020, katika kipengele cha ‘Video bora ya muziki’ kwenye ngoma aliyoshirikishwa na Beyonce ya ‘Skin Girl’.
WizKid alichukua Tuzo ya pili ya Grammy mwaka 2022 katika kipengele cha ‘Favorite Afrobeats Artist’.