pmbet

Nilitaka kurudi Barcelona - Messi

Eric Buyanza

April 19, 2025
Share :

Nyota wa Inter Miami, Lionel Messi, amekiri kwamba alitamani kurejea Barcelona, ​​lakini haikufanikiwa.

Messi alitamani kurejea kwa wababe hao wa LaLiga baada ya Kombe la Dunia la 2022 nchini Qatar.

"Nilikuwa na nia ya kurejea Barcelona, sehemu ambayo siku zote nilitaka kuwepo lakini haikuwezekana tena," Messi aliiambia Simplemente Fútbol.

"Nilikuwa wazi sikutaka kwenda kwenye timu nyingine yoyote ya Ulaya” 

Messi anasema baadae swala la kuamua ni klabu gani aende akacheze ikabidi liwe swala la kifamilia.

Messi aliitumikia Barca kwa misimu 17, akishinda jumla ya mataji 35, yakiwemo mataji kumi (10) ya Laliga na manne (4) ya Ligi ya Mabingwa.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet