Nimeamua kuachana na makalio ya bandia - Amber Rose
Eric Buyanza
March 11, 2025
Share :
Mwanamitindo wa Marekani, Amber Rose amefichua kwanini aliamua kuondoa makalio ya bandia aliyokuwa ameweka.
Amber ambaye pia aliwahi kuwa mpenzi wa Rapa mtata Kanye West, alikuwa akiongea hayo kwenye 'podcast' ya Club Shay Shay, ambapo alikiri kuweka makalio hayo wakati ambapo ilikuwa kama fashion kwa wanawake kuwa na makalio makubwa lakini kwa sasa ameyatoa.
"Niliweka makalio ya bandia wakati ilipokuwa fashion kuwa na makalio makubwa ila kwasasa nimeyatoa," alisema Amber Rose.