pmbet

Nimeanza kupaka mkorogo toka Darasa la sita – Nyoshi El Saadat

Eric Buyanza

May 11, 2024
Share :

Mwanamuziki wa kikongo, Nyoshi El Saadat (Rais wa vijana) anasema alianza kuchubua ngozi ya uso wake kwa mkorogo tangu akiwa darasa la sita, hivyo anawashangaa wanaomuona wa ajabu huku akidai kujichubua kwake ni kujipamba kama wanamuziki wengi wa Congo wafanyavyo.

“Sioni ajabu kupaka mkorogo, nimeanza tangu nikiwa darasa la sita hadi leo ni miaka mingi, pia napaka kwa kuwa ni mwanamuziki ninayejua kujipamba nashangaa wanaonishangaa, we huoni yangu ngozi imetulia na kuwa na mvuto kwa sababu natumia vipodozi vya gharama ambavyo mtu mwingine hawezi kumudu gharama hizo.

“Gharama zake ni kubwa, naweza kutumia Mkorogo wa laki tatu hadi tano kwa kuwa nachanganya vitu vingi na naweza kukosa vvote lakini mkorogo lazima uukute kwenye kabati langu la vipodozi,” anasema Nyoshi. 
NMG

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet