pmbet

Nimedumu na Whozu baada ya kuacha 'Drama' za mitandaoni - Wema

Eric Buyanza

November 4, 2024
Share :

Tanzania Sweetheart @wemasepetu  ameweka wazi kilichomfanya aweze kudumu kwenye penzi lake na whozu.

 

Kwa mujibu wa mrembo huyo 'Drama za mitandaoni' ndicho kilichokuwa kinasababisha asidumu kwenye mapenzi lakini sasa ameachana na drama hizo.


Wema amesema kwasasa ana miaka mitatu na Whozu kwenye mapenzi yao, kitu ambacho hapo nyuma ilikuwa nadra sana 'kutoboa' mwaka penzini.


“Siri ambayo wengi hawaijui ndiyo nawapa leo sasa na najua wengi wanajiuliza, nimewezaje kuwa na Whozu hadi leo hii, nimeachana na maisha ya drama za mitandaoni kuhusu mapenzi,”

“Tangu nilipokutana na Chibaba wangu (Whozu) nimeamua kubadilisha mfumo wa mapenzi na ndiyo maana nimekuwa na raha na kudumu nae hadi leo.

 

👉MWANASPOTI
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet