Nimefuata upendo kwa Nandy sio pesa, pesa hata mimi ninazo - Bill Nas
Eric Buyanza
October 22, 2025
Share :

Nyota wa Bongo Fleva, Billnass amesema mapenzi yake kwa mkewe Nandy yaheshimiwe huku akiwachana wanaomfuatilia kwa mabaya katika ndoa yao.
Billnass anasema watu wengi wamekuwa wakidhani uhusiano wake na Nandy ni kwa sababu ya pesa za mwanadada huyo anayefanya vizuri katika Bongo Fleva na si mapenzi na hapa ameamua kuweka wazi kila kitu ikiwamo tetesi za kuachana.
Billnass anasema ndoa yao inawaumiza wengi na wanatamani waachane na ndiyo maana wanaleta maneno mengi, lakini anachojua wao wako vizuri na hazuii watu kuongea.
Hivi kwa nini watu hupenda kusema nimefata pesa kwa Nandy? Yaani wananichukuliaje? Ujue huwa nawashangaa sana watu hao, halafu nifuate pesa kwa Nandy kwani amekuwa benki? Halafu watu hao wanaosema hivyo ni wazi watakuwa masikini sana kwa sababu sijawahi ona Nandy kama ana pesa sana"
Anaendelea kusema; "Sasa mimi watu kama hao mimi nawezaje kujibishana nao wakati nimeshajua tatizo lao ni kutokana na kipato chao na kumwona Nandy ana pesa. Embu watu tuheshimiane jamani mimi nimefuata upendo kwa Nandy na sio pesa, pesa hata mimi ninazo."
Alipoulizwa kuhusu kuachana na kurudiana kwa madai ya usaliti Billnass alicheka na kufunguka;
"Lini tumeachana? (Kicheko) hayo ni madai tu kama madai mengine, sasa kwa nini tuachane? halafu kwa nini tusalitiane? Hakuna kitu kama hicho bwana na ndiyo maana hukusikia tumezunguza sehemu tumeachana."
MWANASPOTI





