pmbet

"Nimefurahi sana kupanda treni mpya ya SGR, Raha mustarehe" - JK

Eric Buyanza

July 25, 2024
Share :

Rais mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendeleza ujenzi wa reli ya kisasa (SGR). Kikwete ametoa pongezi hizo Morogoro baada ya kuwasili kwa usafiri wa treni hiyo katika kituo cha stesheni ya SGR Kihonda akitokea Dar es Salaam. 

Katika safari hiyo kiongozi huyo alifuatana na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Adam Malima na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa. 

“Nimefurahi sana kupanda treni hii mpya, raha mstarehe, niliamua makusudi kupanda treni kwa maana ya kuona hatua gani tumefikia …nilipita wakati ule wa matengenezo bado wakati wa ujenzi tulifika mpaka Kilosa kwenda kuona hatua iliyokuwepo na sasa imekamilika mpaka hapa,” alisema Kikwete. 

“Leo (jana) tumetumia mwendo wa saa 1:49 kutoka Dar es Salaam kuja Morogoro na ningekuja kwa gari muda kama huu uliotumika ningekuwa nakaribia Chalinze…unaona faida yake ni kutumia muda mfupi, unaweza kuja Morogoro ukafanya shughuli zako ukamaliza na ukapanda ten treni kurudi Dar es Salaam,” alisema Kikwete. Aliongeza: 

“Unaweza kulala Morogoro ukafanya kazi Dar es Salaam na ukarudi Morogoro na katika mazingira ya kawaida kwa usafiri wa gari hili lisingewezekana kufanyika”.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet