Nimefuta Whatsapp, inatumika kijasusi – Rais wa Venezuela
Eric Buyanza
July 4, 2025
Share :
Rais wa Venezuela Nicolas Maduro amesema katika mahojiano ya kipindi cha televisheni kwamba WhatsApp imekuwa ikitumika kwa shughuli za kijasusi na mauaji ya Wapalestina, na kwa sababu hiyo ameifuta program hiyo kwenye simu yake ya mkononi.
"Nimefuta WhatsApp maishani mwangu, Jukwaa hili linatumiwa kubaini makazi ili kutekeleza mauaji, imekuwa ikitumika kuwashambulia na kuwauwa Wapalestina”
"Walitumia WhatsApp kuwaua wanasayansi wa nyuklia nchini Iran"
Hii si mara ya kwanza kwa Rais Maduro kuikosoa WhatsApp. Mwezi Septemba mwaka jana alisema kuwa programu hiyo ilijihusisha na masuala ya ujasusi wakati kulipokuwa na mvutano baada ya kufanyika uchaguzi huko Venezuela.
Maduro pia amewashauri watumiaji wa mtandao huo kutumia njia nyingine mbadala.