pmbet

"Nimeishi bila kunywa maji wala chakula kwa miaka 16" - Muluwork Ambaw

Eric Buyanza

May 17, 2024
Share :

Kutoka nchini Ethiopia, mwanamke aliyefahamika kwa jina la Muluwork Ambaw, anadai ameishi kwa miaka 16 bila kula au kunywa chochote.

Ni ukweli usiopingika kuwa wengi wetu hatuwezi kuvumilia saa chache tu bila kutafuna chochote, lakini Muluwork anasema aliachana na chakula pamoja na maji akiwa na umri wa miaka 10 baada ya hamu ya kula kutoweka. 

Cha ajabu Ambaw ana afya njema na nguvu nyingi tu za kufanya kazi zake za kila siku. 

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 26 ameshafanyiwa vipimo mbalimbali, na madaktari katika hospitali moja mjini Addis Ababa walithibitisha kwamba hakukuwa na ushahidi wowote wa chakula kwenye utumbo wake wakati wa uchunguzi wao.

Muluwork anasema anakumbuka mlo wake wa mwisho kupita kwenye midomo yake ilkuwa ni Dengu na Injera (chakula maarufu cha Ethiopia) na tokea siku hiyo hamu ya chakula ilipotea.

Kali ya yote Ambaw anasema kwa miaka yote hiyo 16 hajawahi kwenda chooni kujisaidia zaidi ya kutumia bafu tu kwa ajili ya kuoga.

Tumewahi kusikia watu wakidai kuishi bila chakula lakini Muluwork ni mmoja wa wachache wanaodai kuwa hajanywa hata maji kwa miaka hiyo 16, jambo ambalo ni gumu sana kwa watu kuamini.

Kulingana na Guinness Records, muda mrefu zaidi ambao mtu ameweza kuishi bila chakula na maji ni siku 18.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet