pmbet

"Nimejituma kwaajili ya Taifa langu" - Bacca

Sisti Herman

January 29, 2024
Share :

Beki wa timu ya Taifa ya Tanzania Ibrahim Hamad Bacca amesema jambo lililomfanya kuwa na kiwango bora katika michuano ya AFCON mwaka huu ni ukubwa wa mashindano hivyo aliyaendea kwa hamasa, kupambana na kujituma kwa ari kubwa kulingana na ukubwa wa mashindano.

 

“Ushindani ulIkuwa mkubwa kwasababu ni mashindano makubwa kwa hapa kwetu Afrika na nadhani pia timu zilikuwa zimejiandaa vizuri ndio maana mechi zilikuwa ngumu” alianza Bacca alipoulizwa kuhusu michuano kwa ujumla.

 

“Kikubwa ni kujitoa kwasababu hili ni taifa langu, nina haki ya kuhakikisha najitolea kwa asilimia zote kuhakikisha nalisaidia taifa langu na mimi mwenyewe kujiweka sehemu nzuri” aliendelea Bacca kuhusu kiwango chake Afcon.

 

“Tulichojifunza ni namna ya kutumia nafasi tunazopata, hapo ndio tulipozidiwa na wenzetu na kuweza kutuhukumu” alihitimisha Bacca kuhusu mapungufu ya Taifa stars.

 

Bacca ameyasema hayo mara baada ya timu ya Taifa kuwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere baada ya kurejea kutoka Ivory Coast walipokuwa wakishiriki michuano hiyo mikubwa zaidi barani Afrika.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet