"Nimeonewa, nakata rufaa" - Pogba
Sisti Herman
February 29, 2024
Share :
Baada ya mapema leo kukutwa na hatia ilimlazimu kifungo cha kutojihusisha kwa namna yoyote na masuala ya mpira baada ya kwa kuthibitika kuwa na tabia ya kutumia dawa zilizokatazwa michezoni, kiungo wa zamani wa Manchester United, Juventus na timu ya Taifa Ufaransa Paul Pogba ametoa taarifa kwa umma iliyoambatana na uamuzi wa kukata rufaa kwa adhabu hiyo.
anaandika Pogba;
“Leo nimefahamishwa kuhusu uamuzi wa Tribunale Nazionale Antidoping na ninaamini kuwa uamuzi huo si sahihi.”
“Nina huzuni, mshtuko na kuumia moyoni kwamba kila kitu ambacho nimejenga katika taaluma yangu ya uchezaji wa kulipwa kimechukuliwa kutoka kwangu.”
“Nisipokuwa na vizuizi vya kisheria habari kamili itakuwa wazi, lakini sijawahi kuchukua kwa kujua au kwa makusudi virutubishi vyovyote vinavyokiuka kanuni za kupinga matumizi ya dawa za kusisimua misuli.”
“Kama mwanariadha wa kulipwa singeweza kamwe kufanya lolote ili kuboresha uchezaji wangu kwa kutumia dawa zilizopigwa marufuku na sijawahi kuwadharau au kuwalaghai wanariadha wenzangu na wafuasi wa timu zozote ambazo nimechezea, au dhidi yangu.”
“Kutokana na uamuzi uliotangazwa leo nitakata rufaa hii mbele ya Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo.”