"Nisaidieni kumshawishi Rihanna ashiriki kwenye albam yangu" – Dj Khaled
Eric Buyanza
July 11, 2024
Share :
Mwanamuziki na Dj maarufu duniani kutoka nchini Marekani, DJ Khaled amewataka mashabiki wake wamsaidie kumshawishi Rihanna ili akubali kushiriki kwenye albamu yake ijayo.
DJ Khaled alitoa ombi hilo hivi karibuni alipokaribishwa kwenye kipindi cha 'Tonight Show' kinachoandaliwa na Jimmy Fallon.
Akiwa kwenye kipindi hicho DJ Khaled alifichua kuwa amemtumia Rihana wimbo ambao angependa mwanadada huyo ashiriki, na kuwataka mashabiki wamsaidie kumshawishi Rihanna ili akubali kuweka mistari yake kwenye wimbo huo.