pmbet

Nitacheza hadi nifikishe miaka 40 - Mo Salah

Eric Buyanza

May 28, 2025
Share :

Mshambuliaji wa Liverpool Mohamed Salah hajui nini kitatokea pindi mkataba wake mpya wa miaka miwili utakapomalizika lakini anaamini kuwa anaweza kucheza hadi atakapofikisha umri wa miaka 40.

"Nitaacha kucheza nikisikia hisia za kufanya hivyo, lakini ukiniuliza maoni yangu, nadhani naweza kucheza hadi umri wa miaka 39 au 40," alisema katika mahojiano na kituo cha televisheni cha Misri cha ON Sports.

"Sijui kitakachotokea, lakini nina furaha hapa Liverpool na nitabaki hapa kwa miaka miwili ijayo. Kisha nitaona nitafanya nini."
Salah atatimiza umri wa miaka 33 ndani ya wiki chache zijazo.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet