"Nitakuja mahakamani kuwaona waliomuua mwanangu" Baba wa Luke Fleurs
Sisti Herman
April 12, 2024
Share :
Baba Mzazi wa Mchezaji wa Kaizer Chiefs Luke Fleurs, Theo aliyeuwawa na majambazi hivi Karibuni akiwa kwenye kituo cha kujaza mafuta jijini Johannesburg amefunguka kuwa atahudhuria mahakamani siku ya hukumu ya washukiwa waliohusika na kesi ya mauaji ya kijana wake.
“Ni huzuni kuona kuwa watuhumiwa wa mauaji ya mwanangu Luke ni vijana wadogo,ambao wana sehemu kubwa ya maisha yao mbele,na sasa sehemu hiyo itapotea, Nitakuwepo mahakamani kwenye kesi, ningependa kuwatazama usoni wauaji wake, Mimi ndio nilikuwa kocha wa Kwanza wa Luke Fleurs akiwa mdogo,nilianza kumfundisha kwa kutumia mpira wa Basketball,ndio maana alikuwa na uwezo mkubwa wa kupiga mashuti” Theo Fleurs
Mdogo wa Mchezaji huyo ambaye kaizer Chiefs imeamua kustaafisha Jezi namba 26 kwa heshima yake amesema wao kama Familia wamesamehe na wanachotaka kuona ni haki ikitendeka,
Hadi sasa watu 6 wamekamatwa wakihusishwa na mauaji ya mchezaji huyo wa Kaizer Chiefs,ambapo Risasi zilizotumika kwenye tukio zimeonekana kuendana na bastola walizokutwa nazo washukiwa.