"Nitarudi jukwaani hata kwa kutambaa" - Celine Dion
Eric Buyanza
June 12, 2024
Share :
Mwanamuziki mkongwe na maarufu duniani kutokea nchini Canada, Celine Dion amesema hataruhusu vita vyake na ugonjwa unaomsumbua wa (Stiff Person Syndrome) kumzuia kufanya maonyesho ya muziki.
Mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 56, aliyasema hayo kwenye mahojiano na Hoda Kotb na kuapa kwamba ataendelea kufanya maonyesho hata kama atalazimika kutambaa kwenye jukwaa na kuzungumza kwa mikono.
“Nitarudi kwenye kwenye stage, hata ikiwa ni lazima nitambae. Hata ikibidi nizungumze kwa mikono,, nitafanya”.
Mwanamuziki huyo amekuwa akipambana kwa siri na ugonjwa huo unaomsumbua kwa miaka 17, kabla hajaamua kuweka wazi mwaka juzi.