Njia ya Dar City kutwaa Ubingwa wa Afrika hii hapa
Sisti Herman
May 5, 2026
Share :

Michuano ya Basketball Africa League (BAL) 2026 inaingia hatua ya mtoano (playoffs) mwezi Mei jijini Kigali, huku ratiba rasmi ikionyesha pambano kubwa kwa klabu ya Tanzania, Dar City ambayo imepangwa kukutana na mabingwa wakongwe wa Angola, Petro de Luanda.
Dar City inaingia kwenye hatua hii ikiwa na kumbukumbu ngumu kutoka mchezo wa mwisho wa makundi dhidi ya Pretoria Capitals, ambapo ilipata ishindi kwa vikapu 100 kwa 75.
Kwa mujibu wa ratiba ya playoffs:
* Dar City vs Petro de Luanda mchezo wa hatua ya robo fainali unatarajiwa kupigwa katikati ya mwezi Mei
* Washindi wa mechi hizi wataendelea moja kwa moja hadi nusu fainali, hatua ambayo huongeza ushindani na presha kwa kila timu
Petro de Luanda inaingia kwenye mchezo huo ikiwa na rekodi nzuri na uzoefu mkubwa wa BAL, jambo linalowapa hadhi ya kuwa moja ya timu hatari zaidi katika michuano hiyo. Hata hivyo, Dar City bado ina nafasi ya kufanya mapinduzi ikiwa itaimarisha ulinzi na kutumia vyema nafasi za kushambulia.
Mashabiki wa mpira wa kikapu nchini Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla wanatarajia kuona kama Dar City inaweza kubadilisha historia na kusonga mbele dhidi ya wapinzani wao wakubwa.
Playoffs za BAL 2026 zinaendelea kuwa jukwaa muhimu la kuonyesha vipaji vya Afrika, huku timu zikishindana sio tu kwa ubingwa bali pia kwa heshima ya bara zima.





