pmbet

"Njooni uwanjani tuwaonyeshe sisi tuna watu" - Benchikha

Sisti Herman

March 15, 2024
Share :

Mara baada ya kurejea nchini kutokea nchini kwao Algeria alipohudhuria kozi fupi ya siku 5 ya ukocha, Kocha mkuu wa Simba Abdelhack Benchikha amesema wanaanza moja kwa moja kwaajili ya mechi mbili mfululizo ikiwemo ya ligi leo dhidi ya Mashujaa na ijayo ya robo fainali ya ligi ya mabingwa dhidi ya Al Ahly.

 

“Nimerudi kwenye timu yangu, tuna mechi kwenye ligi baada ya hapo tunajiandaa kwa mechi kubwa dhidi ya Al Ahly, utajiandaa na hii mechi vizuri na matumaini kuwa mashabiki wetu watakuja kuwaonyesha Al Ahly kuwa sisi tuna watu nyuma yetu na Mungu akijalia tutashinda na hatutakata tamaa” alisema Benchikha alipoongea na idara ya habari ya Simba.

 

Simba leo watashuka dimbani kuwavaa Mashujaa kutoka Kigoma kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara utakaochezwa Azam Complex Chamazi.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet