pmbet

Nsue, kiraka Mhispaniola anayekimbiza Afcon akiwa na Guinea

Joyce Shedrack

January 23, 2024
Share :

Nahodha wa timu ya Taifa Equatorial Guinea, Emilio Nsue akiwa na umri wa miaka 34, anacheza nafasi ya beki wa kulia akiitumikia klabu ya Primera Federecion Club CF Intercity inayoshiriki ligi daraja la tatu nchini Hispania ndiye kinara wa ufungaji katika Kombe la Mataifa ya Afrika 2023 akiwa na mabao matano.  

Nsue mzaliwa wa Hispania aliwahi kushinda ubingwa wa Euro 2007 U-19 na Euro 2011 U-21 akiwa na timu ya taifa ya Hispania, akicheza pamoja na Dani Parejo, Thiago, Juan Mata, David de Gea na wengineo.

Kwenye mchezo wa pili dhidi ya Guinea-Bissau, Emilio Nsue aliweka rekodi ya kuwa  mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi kufunga hat-trick katika historia ya mashindano ya AFCON.

Katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi, Nsue alifunga mabao mawili katika ushindi wa 4-0 dhidi ya Côte d'Ivoire, ushindi ambao unawaondoa wenyeji kwenye michuano hiyo.

Mkongwe Laurent Pokou ndiye mchezaji pekee aliyewahi kufunga magoli mengi zaidi (7) kwenye hatua ya makundi ya michuano ya AFCON kumzidi Nsue mwenye mwenye matano.

Wanaongoza orodha ya wafungaji AFCON 2023 ni Emilio Nsue akiweka kambani magoli 5 Mualgeria Baghdad Bounedjah goli 3, Msenegali Lamine Camara goli 2 huku wanaofutia wote wakitupia magoli mawili mawili . 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet