Nunez aweka rekodi Uruguay ikishinda Copa Amerika
Sisti Herman
June 28, 2024
Share :
Baada ya kufunga goli moja kwenye ushindi wa 5-0 dhidi ya timu ya Taifa ya Bolivia kwenye michuano ya kombe la Mataifa ya Amerika (Copa America), mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Uruguay Darwin Nunez ameweka rekodi yake ya kufunga akiwa timu ya Taifa kwenye mechi 7 mfululizo.
Uruguay baada ya ushindi huo wa jana imefuzu hatua ya mtoano ya michuano hiyo baada ya kufikisha alama 6 na kuongoza msimamo wa kundi A.