Nyama ya Nyoka ina ladha kama ya Kuku - Lupita Nyong'o
Eric Buyanza
January 13, 2024
Share :
Nyota wa Hollywood na mzaliwa wa Kenya mwanadada Lupita Nyong'o amekula nyama ya nyoka kwa mara ya kwanza alipokuwa ziarani nchini Benin.
Katika video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii inamuonesha mwanadada huyo akiwaandaa mashabiki wake wakae tayari kwani anataka kujaribu kula nyama ya nyoka.
Baada ya hapo anaonekana akiinua mfuniko ili kuwaonesha mashabiki wajionee nyama iliyokuwa imetengezwa vizuri kwa kutumia viungo mbalimbali.
MANENO YAKE:
"Haionekani kutisha kama nilivyodhani....haionekani kama ya nyoka" alisema Lupita huku akijikunja na kujiandaa kuonja nyama hiyo.
"Ina ladha kama ya kuku" alisema Lupita huku akila vipande zaidi baada ya hofu ya awali kutoweka.