Nyanda la Kombe la Dunia atimkia ligi kuu ya Chile.
Joyce Shedrack
July 25, 2026
Share :
Mabingwa wa Chile, Colo Colo, wamemtangaza rasmi kipa mkongwe Vozinha kuwa mchezaji wao mpya kupitia kurasa zao za Instagram.
Rais wa klabu hiyo alithibitisha kukamilika kwa uhamisho huo katika mahojiano na ADN Radio Chile, akisema:
"Tumefikia makubaliano na Vozinha, na atajiunga nasi katika siku chache zijazo. Kila kitu kimekamilika."
Uhamisho huu unaashiria hatua kubwa katika maisha ya kipa huyo mwenye umri wa miaka 40 ambaye alikuwa akicheza katika ligi daraja la pili nchini Ureno kabla ya kung'ara kwenye Kombe la Dunia.
Kupitia kiwango chake bora na maonyesho ya kuvutia katika mashindano hayo, Vozinha amejijengea jina duniani na sasa amepata nafasi ya kujiunga na moja ya klabu kubwa zaidi nchini Chile.





