Nyimbo 2 za Harmonize zilizomvutia Rais Samia
Sisti Herman
May 26, 2024
Share :
Rais Samia Suluhu Hassan amesema amesikiliza nyimbo nyingi alizoimba Harmonize lakini 'Never Give Up' na 'Mtu na Nusu' ndizo zimemkaa kichwani.
"Nimesikiliza nyimbo nyingi alizopiga Harmonize hapa lakini nyimbo mbili zimenikaa sana kichwani. moja 'Never Give Up'usikate tamaa huo wimbo ameupangilia vizuri ameutunga kwa ubunifu mkubwa sana ni wa kweli katika maisha usikate tamaa kwa hiyo huo nimeupenda sana," amesema.
Rais Samia ameyasema hayo jana katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam alipohudhuria uzinduzi wa Albamu ya Muziki wa Mama kutoka kwa Harmonize.
Kwa upande wako wimbo gani wa Konde Boy unakukosha?