Nyoni ajivunia kizazi kipya cha Liverpool
Sisti Herman
September 17, 2026
Share :

Kinda wa Liverpool Trey Nyoni alichapisha kwenye mtandao wake wa kijamii wa Instagram picha yake akiwa na vijana wengine wa akademi ya Liverpool baada ya kuifunga Spurs mabao 3-1 kwenye Kombe la Ligi.
Trey na James McConnell walitawala eneo la kiungo na kucheza kwa kiwango cha juu sana, Rio alionyesha uwezo wake wa kipekee na ari ya juu, huku Lewis Koumas akiibuka kuwa Mchezaji Bora wa Mechi kutokana na juhudi zake kubwa za kuwashinikiza wapinzani.
Hivyo ni baadhi ya vipaji vinavyochipukia kutoka akademi ya Liverpool kwa sasa ambao wamepata bahati ya kuaminiwa na kocha Andoni Iraola na kuwapa fursa kama hii.





